Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Iran katika historia ya Uislamu imekuwa na jukumu lisilo na mfano katika kueneza elimu na maarifa; ni ardhi ambayo wanazuoni wakubwa zaidi wa dini wametoka humo, si tu katika madhehebu ya Kishia kwa kuandika Kutub al-Arba‘a, bali pia vyanzo vikuu vya hadithi vya Ahl al-Sunna, majina yenye athari kubwa zaidi yameibuka kutoka katika ardhi hii tukufu.
Waandishi wa Kutub al-Arba‘a walitoka wapi?
Shaykh Kulayni (mwandishi wa "Usul al-Kafi"):
Kulayni alizaliwa katika kijiji cha Kulin, miongoni mwa vijiji vya zamani vilivyozunguka Hasanabad Fashafuyeh, Tehran, umbali wa kilomita 38 kutoka mji wa Ray, katika zama za Imam Hasan al-Askari (as).
Shaykh Saduq (mwandishi wa "Man La Yahdhuruhu al-Faqih"):
Muhammad bin Ali bin Husayn bin Babawayh al-Qummi, maarufu kwa jina la Shaykh Saduq, alizaliwa mwaka 305 Hijria, katika familia ya elimu na uchaji, mjini Qom.
Shaykh T'usi (mwandishi wa "al-Istibsar" na "al-Tahdhib"):
Abu Ja‘far Muhammad bin Hasan bin Ali al-T'usi, maarufu kama Shaykh – bila sifa nyingine – na Shaykh al-Ta’ifa, alizaliwa katika mwezi wa Ramadhan mwaka 385 Hijria mjini T'us (Khorasan).
Waandishi wa Sahih Sitta (vyanzo vya hadithi vya Ahl al-Sunna) walitoka wapi?
Sahih al-Bukhari, imeandikwa na Muhammad bin Ismail al-Bukhari (194–256 H), alizaliwa Bukhara, iliyokuwa sehemu ya Iran wakati huo.
Sahih Muslim, imeandikwa na Muslim bin Hajjaj al-Nishab'uri, alizaliwa Nishab'ur.
Sunan al-Tirmidhi, imeandikwa na Muhammad bin Isa al-Tirmidhi; mwandishi alizaliwa katika mji uliokaribu na mto Jihun ambao wakati huo ulikuwa sehemu ya Iran.
Sunan al-Nasa’i, imeandikwa na Abu Abdurrahman Ahmad bin Ali al-Nasa’i; alizaliwa katika mji unaoitwa Nasa, ulioko Khorasan Kubwa.
Sunan Ibn Majah, imeandikwa na Muhammad bin Yazid bin Majah, maarufu kama Ibn Majah, alizaliwa katika mji wa Qazvin.
Sunan Abi Dawud, mwandishi wa kitabu hiki ni Sulayman bin Ash‘ath, maarufu kama Abu Dawud al-Sijistani, alizaliwa Sijistan (Sistan).
Maoni yako